DKT. SHEKALAGHE; MOI SHIRIKIANENI NA JESHI LA POLISI KUTOA ELIMU YA KINGA AJALI ZA BARABARANI
Posted on: June 17th, 2026Na, Aisha Swahibu, WAF – Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe ameitaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu kinga dhidi ya ajali, ambazo zimeendelea kuwa chanzo kikubwa cha majeraha yanayohitaji huduma za mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu.
Dkt. Shekalaghe ameyasema hayo katika hafla ya maadhimisho miaka 30 ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Juni 17, 2026 katika ukumbi wa MOI Clients Lounge, jijini Dar es Salaam.
Amesema ushirikiano huo utaleta matokeo chanya ya kupunguza na kuzui ajali za barabarani na kupunguza kiasi cha wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupatiwa matibabu ya mifupa na ubongo na kuokoa nguvu kazi ya Taifa.
Aidha, Dkt. Shekalaghe amewapongeza watumishi wa MOI kwa mchango wao mkubwa katika kuokoa maisha ya wananchi na kuendelea kuiwezesha taasisi hiyo kuwa kinara wa huduma za kibingwa ndani na nje ya Tanzania.
Dkt. Shekalaghe amesisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa watumishi wa kada zote, kuanzia ngazi za juu hadi za chini, ili kuhakikisha huduma bora na endelevu zinaendelea kutolewa kwa wagonjwa na wananchi kwa ujumla.
"Nipo tayari kuendelea kutoa ushirikiano wangu kwa MOI katika juhudi mbalimbali za kuboresha afya za wananchi na kuhamasisha elimu ya kinga dhidi ya ajali," amesema Dkt. Shekalaghe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema katika kipindi cha miaka 30 taasisi hiyo imepata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya, utafiti na mafunzo, huku ikiweka mikakati ya kuendelea kuimarisha huduma zake katika miaka ijayo.
Amebainisha kuwa MOI imeendelea kubuni na kutekeleza huduma mbalimbali za kibunifu, ikiwemo huduma za mkoba na programu ya 'Back Stopping', inayolenga kuanzisha na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika hospitali za mikoa mbalimbali nchini. Mikoa inayonufaika na mpango huo ni pamoja na Arusha, Mara, Kagera, Njombe na Ruvuma, hatua inayolenga kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolazimika kusafiri