DKT. SAMIZI ATOA WITO WA MAZINGIRA RAFIKI YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA NA WANAWAKE
Posted on: May 31st, 2026Na Shaban Juma, Kigoma
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa wito kwa jamii, taasisi za umma na binafsi kushirikiana kuondoa unyanyapaa wa hedhi na kuhakikisha huduma rafiki za hedhi salama zinapatikana kwa wanawake na wasichana ili kuwawezesha kuishi kwa utu, usalama na heshima.
Dkt. Samizi ameyasema hayo leo Mei 30, 2026 katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika wilayani Kibondo mkoani Kigoma, ambapo pamoja na kuhamasisha jamii kuhusu hedhi salama, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya hususan kuboresha mazingira rafiki kwa wanawake na watoto wa kike kupitia ujenzi wa miundombinu ya afya, maji, usafi na mazingira salama ya kujifunzia mashuleni.
Amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita umewezesha kupanuka kwa huduma za msingi za afya na kuboresha miundombinu ya vyoo bora mashuleni na katika vituo vya kutolea huduma za afya, hatua ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kulinda afya, utu na heshima ya wanawake pamoja na watoto wa kike nchini.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyobebwa na kaulimbiu isemayo “Tushirikiane Kuhakikisha Huduma Rafiki za Hedhi Salama kwa Wanawake na Wasichana” (Together for a Period-Friendly World), Dkt. Samizi amesema hedhi ni mabadiliko ya kawaida ya kibayolojia na si ugonjwa wala jambo la kuaibisha, hivyo jamii inapaswa kuondoa mila potofu na unyanyapaa unaowakwamisha wasichana kushiriki kikamilifu shughuli za kijamii na kielimu.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili wasichana nchini, amesema tafiti zinaonesha kuwa asilimia 27 ya wasichana hukosa shule angalau siku tatu kila mwezi kutokana na maumivu au kutosimamiwa vizuri kwa mahitaji ya hedhi, jambo linalowapotezea zaidi ya siku 30 za masomo kwa mwaka na kuathiri maendeleo yao kitaaluma.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu rafiki ya hedhi salama kwa kujenga vyoo bora vyenye huduma ya maji pamoja na vifaa vya kuhifadhia