UTARATIBU WA UHAMISHO WA MWANAFUNZI VYUONI

A. TARATIBU ZA KUFUATWA KWENYE CHUO ANACHOTOKA MWANAFUNZI

  1. Awe amefanya mtihani wa mwisho wa semesta na kufaulu. Mwanafunzi anayetakiwa kurudia masomo ya mitihani ndani ya semesta au mwisho wa semesta hataruhusiwa kuhama.
  2. Mwanafunzi awe na sababu za kimsingi za kuhama chuo, zinazoambatana naidhibiti kama, matatizo ya ugonjwa - barua ya uhamisho iambatanishwe na barua ya daktari inayopendekeza mazingira ambayo mwanafunzi ataweza kufaidika kutokana nahali yake ya kiafya . Inatakiwa kuwe na vidhibiti kuwa amekuwa anahudhuria matibabu siyo kwa siku moja tu , bali kuwepo n a mapendekezo ya daktari ambyo yan jitosheleza.
  3. Awe ni mwanafunzi halalai wa chuo, aliyedahiliwakwa kufuata vigezo vilivyoainishwa kwenyemtala husika.
  4. Awe ni mwanafunzi ambaye amefuata taratibu zote za masomo , kuhudhuria darasani kama inavyotakiwa. Awe ameingia darasani kwa asilimia inayotakiwa hadi muda ambao anaomba uhamisho.
  5. Endapo tatizo ni ada kuwakubwa, aambatanishe “fees structure “ ya vyuo viwili chuo anachohamia na chuo anachotoka.
  6. Awe na barua inayotoka chuo anachotaka kuhamia, inaothibitisha kuwepo kwa nafasi.
  7. Baua yake ya kuomba uhamisho iwe imepitishwa na mkuu wa chuo au kaimu, endapo chuo hakina mkuu wa chuo aliyeteuliwa . Watumishi wengine wasihusike na uhamisho wa wanafunzi.
  8. Barua ya uhamisho iainishe aina yamafunzo ambayo mwnafunzi anachukua na alichaguliwa kwa ngazi gani (NTA Level 6) . Hili lithibitishwe na Mkuu wa Chuo.

B. MUDA WA KUHAMA MWANAFUNZI

  1. Mwanafunzi anaruhusiwa kuhama mwisho wa semesta baada ya kufanya mtihani wa mwisho wa semesta na kufaulu. Hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuhama katikati ya semesta au kama anadaiwa mitihani ya marudio ya semesta.
  2. Kujiunga na masomo wiki ya kwanza ya semesta kwenye chuo anachohamia mwanafunzi.
  3. Mwisho wa semesta ya kwanza (semesta 1) kwa ngazi ya NTA Level 4 na 5 (NTA Level 4 na 5) kwa kozi ya stashahada na mwisho wa semesta ya kwanza ngazi ya 4 kwa kozi ya astashahada (cheti).
  4. Mwanafunzi hataruhusiwa kuhama semesta II (semesta yapi ).
  5. Mwanafunzi atatakiwa kuwepo chuoni akiendelea na masomo wakati wote anapofanya maandalizi y akuhama hadi uhamisho wake utakapokamilika.

C. TARATAIBU ZA KUFUATWA KWENYE CHUO ANACHOKWENDA MWANAFUNZI

  1. Kiwe chuo kilichosajiliwa na Barasa la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).Kinachotoa mafunzo ya aina moja na kile anachotoka mwanafunzi . Ieleweke kwamba mwanafunzi aliyechaguliwa kuchukua mafunzo ya cheti hatahamishiwa chuo cha stashahada,endapo chuo hicho hakitoi ngazi ya cheti.
  2. Mwanafunzi awe anahama kwenda kujiunga na mafunzo ya aina moja na chuo atokacho, kwa mfano:- Mwanafunzi anayechukua mafunzo ya Maabara, atahamishiwa kwenda kuchukua mafunzo hayo hayo na siyo vinginevyo.
  3. Mkuu wa chuo athibitishe kuwepo kwa nafasi ya masomo kwa maandishi kwa kuzingatia vipengele A na B.
  4. Barua ya chuo inayoainisha muda wa kuanza muhula wa masomo na kumaliza. Nakala ya barua hiyo na kalenda itumwe Wizarani.

D. NAMANA YA KUANDA KWA UHAMISHO

Mwanafunzi ambaye anasababu ya msingi ya kuhama kama ilivyo ainishwa hapo juu anatakiwa afanye yafuatayo:-

  1.  Atoe taarifa kwa maandishi , kwa Mkuu wa chuo ya kusudio la kutaka kuhama chuo yenye sababu za msingi na vielelezo kama ilivyoainishwa hapo juu.
  2. Endapo mkuu wa wa chuo ataridhia sababu za mwanafunzi zenye vithibitiaho , Mkuu wa chuo amwelekeze mwanafunzi jinsi ya kuandika barua na kumpitihshia barua hiyo,nakala ya barua hiyo na vudhibitisho itumwe wizarani.
  3. Mkuu wa chuo ambacho mwanafunzi huyo anatorajia kuhamia,anatakaiwa kumpa jibu mwanafunzi kupitia kwa mkuu wa chuo alichoko, kwa kuzingatia taratibu zilizoaininshwa hapo juu.

E. ZINGATIA

  1. Mwanafunzi hapaswi kuja wizrani na kusubiri barua nje ya taratibu zilizoainishwa hapo juu. Pia uhamisho kama maombi mengine ,yanaweza kukubaliwa au kukataliwa. Hivyo hakuna sababu ya mwanafunzi kuwasilisha barua Wizarani na kusubiri majibu. Majibu yote yatapita kwa wakuu wa vyuo.
  2. Hakuna mwanafunzi atakaye hamishwa kwa kukariri semesta iliyopita,au mwaka wa masomo uliopita, iwapo mwanafunzi huyo hajatakiwa kufanya hivyo kwa taratibu zilizopo.
  3. Mwanafunzi atakaye hamishwa akiwa na masomo ya kukariri (Supplementary) anatakiwa kufaulu mitihani yake ya supplementary ndipo ahame chuo kwa utaratibu ulioainishwa katika vipengele A na B
Go to top