BARAZA LA WATAALAM WA AFYA YA MAZINGIRA
(The Environmental Health Practitioners’ Registration Council)
UTANGULIZI
Baraza la Kusajili Wataalam wa Afya ya Mazingira limeundwa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria Na.20 ya Kusajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira ya Mwaka 2007 “The Environmental Health Practitioners (Registration) Act No. 20 of 2007”. Baraza lilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 20 Novemba, 2009 na Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria ya Usajili na kanuni zilizotungwa chini yake The Environmental Health Practitioners (General) Regulations, 2011 Kanuni ya 3,4 na 5 Wataalam wote wanatakiwa kusajiliwa, kuandikishwa na kuorodheshwa.
MAMLAKA YA BARAZA
Baraza lina mamlaka ya kusajili wataalam wote na huduma mbalimbali za afya ya mazingira kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Kusajili ya Wataalam wa Afya ya Mazingira na Kanuni ya 19 ya Kanuni za Kiujumla zilizoundwa chini ya Sheria ya Kusajili Wataalam wa Afya ya Mazingira.
UTARATIBU WA KUSAJILI
Wataalam wote wa Afya ya Mazingira na huduma za afya ya mazingira zitatakiwa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zilizowekwa. Wahusika watatakiwa kujaza fomu na nyaraka kabla ya usajili. Aidha, wakati wa urejeshaji fomu wahusika watatakiwa kuambatisha vyeti vya taaluma, vibali (watoa huduma za Afya ya mazingira) na slipu ya benki inayoonyesha malipo.. Fomu na vyeti vilivyothibitishwa viwasilishwe ofisi ya Msajili kwa njia ya posta au zinaweza kuwasilishwa na mhusika mwenyewe.
WAFANYAKAZI WA BARAZA
- Bw. Iddi L. Hoyange (Msajili), MBA, LLB,DEHS
- Bw. Adolf V. Kiyunge, BSc. EPM, DEHS
- Bi. Mariam Mahamudu, BSc. EHS
FOMU ZA MAOMBI YA USAJILI NA GHARAMA ZA KAZI MBALIMBALI
- Kiambatanisho cha kwanza (Majukumu ya Mtaalam wa Afya ya Mazingira)
- Kiambatanisho cha pili (Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira)
- Kiambatanisho cha tatu (Maombi ya Leseni ya Wataalam wa Afya ya Mazingira)
- Kiambatanisho cha nne (Maombi ya leseni za kutoa huduma mbalimbali za afya ya mazingira)
- Kiambatanisho cha tano (Gharama zitakazolipwa kwa shughuli mbalimbali
Download Ducuments:
Environmental Health Practitioners Council