Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akionesha moja ya fomu ya usajili wa dawa za tiba asili kundi la pili ,uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa wizara,kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili/Mbada Dkt. Edmund Kayombo.

Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa fomu hizo ambazo litatumiwa na waganga wa tiba asili/mbadala watakaogundua dawa.

Katika uzinduzi huo pia Waziri Ummy alizindua kadi mpya ya  chanjo ya Manjano(yellow Fever),pichani akionesha utofauti wa kadi za zamani na kadi mpya,ambapo amewasihi wananchi kuacha kuwatumia vishoka kupata kadi hizo bali kwenda kwenye vituo maalumu vinavyojulikana vinatoa chanjo hiyo,kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Otilia Gowele

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akionesha mfano wa kadi hiyo ambayo ina kurasa nyingi tofauti na kadi ya zamani(picha na Wizara ya Afya)

Feature News & Events

Go to top