Home
 
Roles
 
Organisation Structure
 
Programmes & Projects
 
Agencies & Associations
 
Regulatory Bodies
 
Health Facilities
 
Health Facility Registry
 
Health Services
 
Health Indicators
 
Diseases Report
 
Documents
 
Links
 
Tenders
 
Staff Webmail
     
   
     
 
Home > News in Detail
22nd January 2010

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

 

 

TANGAZO LA KAZI

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

 

1.                  AFISA TAWALA DARAJA LA II (Nafasi 1)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-

                                            i)            Utawala

                                          ii)            Elimu ya jamii

                                        iii)            Sheria (baada ya intership)

                                        iv)            Maenejimenti ya Umma

                                          v)            Uchumi

                                        vi)            Na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

 

(b)        Kazi za Maafisa Tawala

                                            i)            Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali

                                          ii)            Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji katika Ofisi za Serikali

                                        iii)            Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu

 

(c)         Mshahara

 

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

                    

                     Kituo cha Kazi:   Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam.

 

2.                  AFISA UTUMISHI DARAJA II –Nafasi (1)

(a)         Sifa

kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi Jamii au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambliwa na serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:

·        Menejimenti ya Raslimali Watu (Human Resources, Management)

·        Elimu ya Jamii (Sociology)

·        Utawala na Uongozi (Public Administration)

·        Mipango ya Watumishi (Manpower Planning)

Wawe na ujuzi wa kutumia computer

 

 

 

(b)        Kazi za kufanya

i)       Kutunza Kumbukumbu sahihi za Watumishi wote katika Wizara.

ii)      Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya Utumishi

iii)     Kutafiti, kuchanganua na kukadiria idadi ya Watumishi wanaoihitaji mafunzo

iv)     Kuandaa na kupanga Mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu

v)      Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya mafunzo kwa kushirikiana na vyuo vilivyopo chini ya sekta ya Afya

vi)     Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu Mipango ya Watumishi

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Kituo kazi:- Makao Makuu ya Wizara

 

3.                  MCHUMI DARAJA LA II (Nafasi 4)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika Uchumi (Economics Project Planning and Management, Economics Policy Planning and Management)

 

(b)        Kazi za kufanya:

                                            i)                  Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa Sera na Mipango za Afya na Ustawi wa Jamii.

                                          ii)                  Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yatokanayo na utekelezaji wa Sera za Afya na Ustawi wa Jamii.

                                        iii)                  Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya uchumi jumla.

                                        iv)                  Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika Sekta ya Afya

                                          v)                  Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha  vipaumbele vya ustawi na maendeleo ya jamii.

                                        vi)                  Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za masuala ya sekta ya Afya kwa Washikadau.

                                      vii)                  Kuchambua na kutafsiri (Interpret) takwimu na taarifa mbalimbali za Afya.

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma

 

Kituo cha Kazi: Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam.

 

4.                  MTAKWIMU DARAJA LA II. (Nafasi 4) 

           

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia ‘Information Communication Technology (ICT).

 

(b)        Kazi za Kufanya

i)           Kubuni na kuendeleza mfumo wa Kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu za Afya.

ii)                     Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua takwimu za mifano/vielelezo “ sampling”

iii)                Kukusanya, kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Kituo cha Kazi: Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam

 

5.                  AFISA USTAWI  WA JAMII DARAJA LA II (Nafasi  24)

 

(a)         Sifa :-

Kuajiriwa wenye Shahada ya Kwanza (B.A, in Social Work or Sociology) au Sashahada ya Juu ya Ustawi wa Jamii ( Advanced Diploma in Social Work) kutoka Chuo  kinachotambuliwa na Serikali.

 

(b)        Kazi za Kufanya:

                                            i)                  Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, watoto na washtakiwa).

                                          ii)                  Kufanya ukaguzi wa mazingira wnayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili.

                                        iii)                  Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.

                                        iv)                  Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii.

                                          v)                  Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee, malei ya watoto na familia zenye matatizo.

                                        vi)                  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vyuo vya walezi wa watoto wadogo mchana.

                                      vii)                  Kupokea, kuchambua na kundaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akinmm waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.

                                    viii)                  Kupokea, kuchambua na kuanda orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.

                                        ix)                  Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.

                                          x)                  Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa

                                        xi)                  Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi vya watu wenye ulemavu, Mahabusi za Watoto na Shule za Maadilisho.

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya Kazi:  Hospitali ya Kibongoto, Chuo cha Malezi Kisangara Same, Shule za Maadilisho Irambo - Tabora na Mbeya na Ofisi za Ustawi wa Jamii katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida, Shinyanga, Mwanza, Ruvuma, Kagera, Rukwa, Iringa na Mbeya.

 

6.                  MCHAMBUZI MIFUMO YA KOMPYUTA DARAJA  II (Nafsi 7)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya sayansi ya Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

 

(b)        Kazi za kufanya

                                            i)            Kuweka kumbukumbu za utaratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.

                                          ii)            Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na udhibiti unaohusu Kompyuta

                                        iii)            Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara.

 

(c)            Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

                        Vituo vya Kazi: Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Chuo cha CEDHA       – Arusha, PHC-Iringa na Muhimbili Complex       

 

7.                  MKUTUBI DARAJA LA II – NAFASI (1)

(a)         Sifa

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani ya Ukutubi au sifa inayolingana na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotabuliwa na Serikali

 

(b)        Kazi za kufanya

i)       Kupanga ratiba ya kazi kwa watumishi walio chini yake

ii)      Kuwaelekeza kazi Wakutubu Wasaidizi

iii)     Kuhakikisha kuwa maktaba ni safi

iv)     Kufanya kazi nyingine za maktaba atakazopangiwa na mkuu wa kituo

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. D kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Kituo cha kazi:- CEDHA Arusha

 

 

8.                  AFISA UGAVI MSAIDIZI DARAJA LA II (Nafasi 14)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye Cheti cha ‘National Store – Keeping Certificate, au ‘Foundation Certificate’ kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.

 

(b)         Kuajiriwa wenye Diploma ya kawaida ‘Ordinary Diploma in Materials Management’ kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.

 

(c)         Kazi za Afisa Ugavi Msaidizi

                                            i)            Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.

                                          ii)            Kupokea vifaa vipya vitakavyotolewa na wazabuni mbali mbali na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.

                                        iii)            Kufungua na kutunza ‘Bin Card’ kwa kila kifaa kilichopo ghalani.

                                        iv)            Kufungua ‘Ledger’ ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.

                                          v)            Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.

                                        vi)            Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.

                                      vii)            Kuandaa hati za kupokelewa vifaa.

                                    viii)            Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa.

                        

(d)        Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya kazi: Njombe NTC, Mafinga NTC, Nachingwea NTC, Nzega NTC, Kibondo NTC, Korogwe NTC, Kigoma COTC, Kagemu EHS, Musoma COTC , Kiomboi NTC, AMO Mbeya, Kilosa COTC, Mpwapwa EHS na Geita NTC

 

9.                  KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (Nafasi 15)

 

(a)         Sifa :-

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.  Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

 

(b)           Kazi za Kufanya

                                                  i)            Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.

                                                ii)            Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kusaidiwa.

                                              iii)            kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni taarifa za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumwarifu Mkuu wake kwa wakati anaohitajika.

                                              iv)            Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.

                                                v)            Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

                                              vi)            Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

                                            vii)            Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi   

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya Kazi:   Pharmacy Council, Kondoa NTC, Njombe NTC, Korogwe NTC, Mafinga NTC, Nachingwea NTC, Nzega NTC, Kibondo NTC, Mtwara COTC, Singida Lab., Mpwapwa EHS, Mkomaindo NTC, Kilosa COTC, Geita NTC na CEDHA Arusha.

 

10.             MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (Nafasi 4)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne wenye Cheti cha Utunzaji kumbukumbu katika  fani ya Masjala.

 

(b)        Kazi za Kufanya

                                            i)                  Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji

                                          ii)                  Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka

                                        iii)                  Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classfication and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi

                                        iv)                  Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu

                                          v)                  Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili

                                        vi)                  Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya Kazi:  Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali Malumu ya Mirembe Dodoma, CEDA Arusha na Mbeya Theatre Management.

 

11.             MSAIDIZI WA MAKTABA DARAJA LA II ( Nafasi 5)

           

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wenye cheti cha Mitihani wa Taifa wa kidato cha IV ambao wamefaulu mafunzo ya Wasaidizi wa Mktaba (National Library Assistants Certificate Course) yatolewayo na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania au wenye cheti kinacholingana na hicho.

     

(b)        Kazi za Kufanya:

i)           Kuandikisha wasomaji

ii)                     Kupanga vitabu katika rafu (Shelves)

iii)                Kuazimisha na kupokea vitabu vinavyoazimwa

iv)                Kukarabati vitabu vilivyochakaa

v)                     Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Kituo.

                             

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya Kazi:  Nzega NTC, Kibondo NTC, Nachingwe NTC, Mbeya Theatre Management na Kilosa COTC

 

 

 

12.             FUNDI SANIFU (UJENZI) DARAJA LA II - Nafasi 1

 

(a)            Sifa :-

i)                    Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zilizotajwa hapo juu.

ii)                  Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi za ufundi za miaka mitatu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zilizotajwa hapo juu..

iii)                Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zilizotajwa hapo juu.

iv)                Wenye Stashahada ya kawaida katika fani za ufundi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

 

(b)           Kazi za Kufanya

                                                i).                  Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba, kupaka rangi na kufunga mabomba;

                                              ii).                  Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani ‘furniture’

                                            iii).                  Kufanya kazi za upimaji (survey) wa majengo kama atakavyoelekezwa;

                       

(c)            Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS.C kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Kituo cha kazi:- Makao Makuu ya Wizara

 

13.             MPIGA CHAPA  MSAIDIZI – NAFASI (4)

 

(a)         Sifa

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI katika masomo ya sayansi , au Sanaa, wenye Cheti cha Majribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test GradeI ) katika ‘Lithography/Composing/Binding/Machine Minding’, au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya kupiga chapa kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

 

(b)        Kazi za kufanya

                                            i)            Kukunja karatasi ngumu na kutengenenza ‘covers’ za vitabu, majarida , madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora.

                                          ii)            Kukurabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika

                                        iii)            Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipomo vyake au katika seti

                                        iv)            Kuendesha Machine za kukata karatasi/kupiga chapa/Machine za ‘Composing’, kushona au kugandisha vitabu , majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo wa ubora wake.

                                          v)            Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya kazi:- HEU Dar es Salaam na CEDHA Arusha

 

14.             MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (Nafasi 4)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa kwa wahitimu wa Kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya maarifa ya nyumbani (Home Craft Management) au mafunzo yanayofanana na hayo, au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya Ustawi wa jamii.

 

(b)        Kazi za Kufanya

                                            i)            Kulea watoto katika vituo vya kulelea watoto mchana.

                                          ii)            Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya watoto wadogo.

                                        iii)            Kusaidia shughuli za Kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la kituo.

                                        iv)            Kuwa Kiongozi wa kituo cha kulea watoto.

                  

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGS. B kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya Kazi: Makazi ya Wazee ya Nunge - Dar es Salaam, Chuo cha Watoto yatima Kurasini, Chuo cha watu wenye ulemavu cha Masiwani Tanga, Chuo cha Watu wenye Ulemavu Singida.

 

15.             MSAIDIZI WA OFISI –NAFASI (1)

(a)         Sifa

Kuajiri wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

 

(b)        Kazi za kufanya

i)          Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.

ii)         Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha sehemu  zinazohusika.

iii)        Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa

iv)        Kutayarisha chai ya ofisi

v)         Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka posta

vi)        Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili

vii)       Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni na kuyafunga baada ya saa za kazi

vii)       Kudurufu barua au machapisho kwenye Machine za kudurufia

viii)      Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo

ix)        Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika

 

 

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGOS. A kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Kituo cha kazi:- Makao Makuu ya Wizara

 

16.               MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II ( Nafasi 33)

 

(a)         Sifa:-

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu.

 

(b)        Kazi za kufanya

                                            i)            Kusafisha vyombo vya kupikia.

                                          ii)            Kusafisha vyombo vya kulia chakula.

                                        iii)            Kusafisha  meza itumiwayo kulia chakula.

                                        iv)            Kuwatayarishia Wapishi/Waandalizi vifaa vya Mpishi na Mezani.

                                          v)            Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.

                                        vi)            Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.

                  

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGOS. A kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

                     Vituo vya Kazi: Nachingwea NTC, Kibondo NTC, Nzega NTC, Kondoa NTC, Same NTC, Bagamoyo NITC, Njombe NTC, Musoma COTC, Korogwe NTC, Kigoma COTC, Kiomboi NTC, Kagemu EHS, Mtwara NTC, Lindi COTC, Mafinga COTC, Kilosa COTC, Muheza VCT, Mpwapwa EHS, Mkomaindo NTC, Sumbawanga COTC, Mirembe NTC, Geita NTC, Mtwara COTC.

 

17.             MLINZI – Nafasi (48)

 

(a)         Sifa

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/Polisi/JKT au Mafunzo ya Zima moto kutoka katika chuo knachotambuliwa na Serikali

 

(b)        Kazi za kufanya

i)          Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini

ii)         Kuhakikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.

iii)        Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku

iv)        Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi

v)         Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo

vi)        Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika, kama vile Polisi na Zimamoto.

vii)       Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi

 

 

(c)         Mshahara

Mwajiriwa atalipwa ngazi ya mshahara ya TGOS. A kulingana na Muundo wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma.

 

Vituo vya kazi:-  Nachingwea NTC, Kibondo NTC, Nzega NTC, Musoma COTC, Kiomboi NTC, Mtwara NTC, Lindi COTC, Masasi COTC, Mafinga COTC Mpwapwa EHS, Mkomaindo NTC, Ngudu HO, Kilosa COTC, Mtwara COTC, Chuo cha Ufundi wa Stadi za Kazi Yombo, Mahabusi ya Watoto-Upanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Nunge, Makao ya Watoto Kurasini, Makazi ya Wazee na wasiojiweza Kibirizi, Chuo cha Kisangara –Same, Makazi ya Wazee na wasiojiweza Njiro na Mahabusi ya Watoto Moshi.

 

Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45

 

Barua zote za Maombi ziandikwe kwa mkono  na ziambatanishwe na:-

1.      Maelezo binafasi (CV) ya mwombaji

2.      Nakala za Vyeti vya Kidato cha nne na cha sita

3.      Vyeti vya taaluma inayohusika na kazi inayoombwa.

4.      Nakala mbili za picha za mwombaji za hivi karibuni.

 

Barua zote za maombi zitumwe kwa:-

 

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM.

 

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe: 31/01/2010

 

 

 

 

 

 
 
judfhdsjf
© 2005 Ministry of Health and Social Welfare