Home
 
Roles
 
Organisation Structure
 
Programmes & Projects
 
Agencies & Associations
 
Regulatory Bodies
 
Health Facilities
 
Health Facility Registry
 
Health Services
 
Health Indicators
 
Diseases Report
 
Documents
 
Links
 
Tenders
 
Staff Webmail
     
   
     
 
Home > News in Detail
9th October 2009
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kibali cha Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imepewa Mamlaka ya kuwapangia vituo vya kazi wahitimu wa kada za afya kwa kuzingatia ikama iliyoidhinishwa kwa ajili ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

Wahitimu wote wa kada mbalimbali za Afya mnaombwa kuwasilisha barua zenu za maombi ya kupangiwa vituo vya kazi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuanzia tarehe ya Tangazo hili.

Sifa za mwombaji:
  1. Awe ni raia wa Tanzania

  2. Awe na umri usiozidi miaka 45.


Maombi yote yaambatanishwe na:-
  1. Nakala ya Cheti cha Taaluma

  2. Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita

  3. Maelezo binafsi (CV)

  4. Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni

  5. Nakala ya cheti cha usajili


  6. Nakala ya vyeti vya Taaluma na vyeti vya Kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu au Wakili.

    Barua zote zitumwe kwa:-

    Katibu Mkuu
    Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
    S.L.P. 9083
    DAR ES SALAAM
 
 
judfhdsjf
© 2005 Ministry of Health and Social Welfare